By Debora K. Mwangosi
Nini maana ya Imani?
Imani ni kuamini kinachofanana na kusadiki, lakini pia Imani imetafsiriwa katika vitabu vya dini ya Kikristo na ya Kiislamu.
Katika dini ya Kikristo, Imani maana yake ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana. Maana hii imetoka katika kitabu cha Waebrania sura ya 11 mstari wa 1.
Na katika dini ya Kislamu Imani maana yake ni kusadiki au utambuzi unaoambatana na kukubali pia kufuata muelekeo wa kidini. Hivyo neno Imani limeanza kutumika tokea kwenye dini ambazo tunaziamini, na ukisoma katika vitabu vyote viwili ya dini utaona kwa namna gani Imani ilikuwa inawasaidia sana katika kutimiza haya za mioyo yao ama shida zao.
Sababu ambazo watu wengi sana wanashindwa kujiamini katika maisha.
1. kupenda kushindana.
Katika dunia tunayoishi sasa hivi kumekuwa na ushindano wa ajabu sana hususani wa watu kuonesha kuwa wanaishi maisha mazuri wanapokuwa katikati ya jamii. Kutokana na hali ya ushindani ambao umeteka maisha ya watu wengi sana inapelekea hali ya kutokuwa na Imani juu ya maisha yao na kushindwa kujiamini. Kwasababu wanakuwa wanataka kuishi maisha ambayo siyo yao.
2. Hofu.
Mtu yoyote mwenye Imani katika maisha yake basi hali ya hofu haina nafasi ndani yake, moja ya kigezo cha kuwa na Imani ni ujasiri mto yeyote mwenye Imani ni jasiri sana katika kila kitu ambacho anafanya. Kutokana na maisha ya watu wengi kutawaliwa na hofu ya kushindwa katika maisha hupelekea hali ya kutojiamini kuongezeka, yote haya inasababisha na kutokuwa na Imani na maisha unayoishi.
3. Tambua picha ya maisha yako.
Huwezi fanikiwa katika maisha yako kama hujabeba picha ya maisha ambayo unataka kuishi, na mafanikio ya mtu yoyote yanaaza na picha ambayo ipo ndani yake na badae huja kudhihirika katika hali ya uhalisia na kuonekana. Watu wengi sana ambao wanashindwa kuwa na picha ya maisha yao wanakuwa na hali ya kutojiamini, lakini pia Imani ndo msingi wa kila kitu ukishajiamini kaweka Imani na malengo yako na jitihada zako katika maisha yako basi jua kwamba huwezi kukabiliana hali ya kutojiamini.
4. Aina ya watu wanaokuzunguka.
Unaweza sema kuwa unaimani lakini je Imani yako inaimarishwa na aina gani ya watu wanaokuzunguka. Katika safari ya kiroho na kimwili ni muhimu sana kuchagua watu ambao unataka wakuzunguke siyo kila mtu utamuhitaji katika maisha yako. Hivyo basi Imani yako itazidi kuwa imara kama watu wanaokuzunguka wanaamini au wanamaono kama wewe mfano unawatu ambao wanaimani na kufanikiwa au kuwa tajiri sasa kama wewe umebeba Imani ya kuwa na mafanikio alafu unakaa na watu wenye Imani tofauti na wewe ni changamoto kufanikiwa na kuepuka hali ya kutojiamini.
5. Penda kuishi kwa wakati uliopo.
Silaha moja wapo kuweza kujiamini katika maisha ni kuishi kwa wakati uliopo katika safari ya maisha kupanda na kushuka ni moja ya nyakati ambazo kila mwanadamu mpambanaji anapitia, na katika nyakati hizo unakuwa unafundishwa vitu mbalimbali ukishindwa kuishi katika wakati uliopo basi jua kwamba utakosa hali ya kujiamini na kama awali nilivyosema kujiamini inaletwa na Imani ambayo ipo ndani yako.
Faida ya kuwa na Imani.
1. Huleta nuru.
Imani ni nuru katika maisha ya mwanadamu kwasababu inakuwa inasaidia kufanikisha malengo yako ambayo unayo katika maisha yako. Hivyo basi Imani inasaidia sana katika njia ya mafanikio.
2. Huchochea mafanikio.
Imani ni moja ya msaada katika mafanikio, kwasababu unakuwa na uwezo wakuthubutu kile ambacho unakiamini na kuweza kukionesha katika uhalisia. Huwezi kufanikiwa kama hauna maono au ndoto na Imani juu ya ndoto ya mafanikio ambayo unayonadani yako. Kupitia Imani inakuwa inachochea mafanikio yako.
3. Ukaribu na Mungu.
Kama ambavyo tumefahamu maana ya Imani kutoka kwenye vitabu vyetu vya dini, jua kwamba muda mwingine mafanikio yako katika maisha yako yanatokana na Imani ambayo ipo ndani yako. Na Mungu hutenda au kukujibu changamoto au maswali yako huangalia Imani ambayo ipo ndani yako, ukisoma vizuri vitabu vya dini utaona Mungu hapatani na watu wenye Imani haba juu yake.
HITIMISHO.
Ninachojua katika dunia hii kila mwanadamu anaimani yake inaweza kuwa anaamini katika dini ambazo metoka kuziongelea ama vinginevyo. Lakini jua kwamba kuwa na Imani ni moja ya sehemu ya maisha huwezi kuwa unaendesha maisha yako bila kujua ni nini unaamini katika safari yako. Ni muhimu sana kusimamia katika kile unachokiamini lakini tu ukiwa na uwahika kuwa Imani yako itakusaidia katika safari yako ya maisha.