By Maureen C. Minanago
Hofu ya mwanadamu hutofautiana kwa ukuu. Lakini sote huogopa kwa namna fulani. Hata mwenye nguvu wanamaeneo yao ya unyonge.
Tuogope yote lakini tusiogope kusema ukweli inapobidi, na si ukweli tu ila kuzungumza kwa ujumla.
Wapo wenye mawazo mazuri sana ambayo yasipokaliwa kimya yanaweza kuleta athari kubwa tu kwa mtu mmoja au jamii nzima.
Yamkini ukambadilisha mtu / watu, ukaokoa maisha ya mtu / watu, ukapata msaada ulioukusudia au kuutamani kwa muda mrefu, ukatambulika katika familia, ukoo, eneo, nchi, bara au dunia kwa kusema kwako.
Usisite, usikate tamaa, usiogope kusema sababu yule ni mtu mzima, yule ni mkali, yule ni mpole sana, yule haeleweki, yule simuamini. Usihisi labda hivi, labda vile. Sema usikike hata kama utamkwaza, hata kama utamuudhi, hata kama atakujibu vibaya, atakukaripia, atakutukana ama atakukalia kimya. Katika yote, hakika kuna ambalo litamgusa na kumbadilisha japo kidogo.
Kama ni cha thamani kiseme…kitaleta mabadiliko!! Kiseme, moyo wako uridhike pia!!
Katika sehemu ya tatu, kifungu cha 18 cha Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977, tunaona kuwa kila mwanadamu anauhuru wa kuongea / kuzungumza. Kumbe basi, ni wajibu wa kila mmoja kuzungumza kile anachoona ni sahihi, ilimradi tu asiseme uongo wala kuzusha jambo.
Usiogope!!