By Maureen C. Minanago
Maziwa mtindi yanavirutubisho vingi sana vinavyopendkezwa kuwa na faida nyingi katika mwili wa binadamu.
Ni lini mara yako ya mwisho kupata maziwa mtindi? Pata kama chakula ama baada ya chakula ama kabla ya chakula, yatakusaidia. Soma faida zake hapa.
Kabla ya kuzifahamu faida ya maziwa mtindi kwanza tuone virutubisho vichache vinavyopatikana ndani yake. Mtindi una calcium, phosphous, riboflavin (vitamin B2), iodine, vitamin B12. panantothenic acid (vitamin B5) zinc, potassium pamoja na molybdenum. Mbali na virutubisho hivyo, maziwa mtindi pia yana wadudu ambao ni “bakteria hai” wenye umuhimu mwilini kiafya.
Kuna homoni (cortisol) sehemu ya katikati ya tumbo na kiuno ambayo inakazi ya kuamuru ubongo kuongeza mafuta chini ya tumbo hivyo kusababisha kitambi.
Maziwa mtindi husaidia kupunguza ama kuondoa kabisa kitambi
Kwa asilimia 82; kwa msaada wa madini ya calcium yaliko kwenye mtindi ambayo hupunguza homoni inayoamuru mafuta kwenda chini ya kiuno.
Ni vema kunywa kutumia maziwa mtindi mara moja moja hasa wakati wa jioni unapokuwa umepumzika yaani baada ya shughuli zako.
Pata mtindi ukiambatanisha na maji mengi ili kurahisisha mfumo wa upatikanaji wa maji mwilini. Mtindi huufanya mwili kuwa na maji muda wote yaani usiwe mkavu. Faida zingine ni pamoja na:
Kurefusha Maisha
Kwani yanauwezo wa kupambana na magonjwa.Ni kinga kwa kina mama kwani inakinga dhidi ya maradhi ya kuambukiza ukeni (vaginal infections).Ni kinga ya mwili kwani inapambana na magonjwa kama saratani mfano saratani ya utumbo.Kuondoa lehemu (cholesterol) mbaya mwilini hilo kumuepusha mtu na tatizo la shinikizo la damu.Kupunguza uzito kwa asilimia 22 kwani yanapunguza mafuta mwilini.Yanasaidia kukupa seli za misuli yako kupitia virutubisho vya protini.Yanasaidia kuupa mwili nguvu kupitia virutubisho vya wanga.Chonde: Usitumie maziwa ya mtindi yatokanayo na maziwa ya unga kwani utakosa ule uchachu na bakteria hai wenye umuhimu mwilini, hivyo kukosa virutubisho mwilini.
Unaweza pata maziwa mtindi kama mboga ukala na ugali, unaweza kuyanywa yenyewe kama chakula, unaweza kuyanywa na kitafunwa kama biskuti, mkate au maandazi.
Wengi wetu hupenda kupunguza miili kwa mazoezi lakini jambo kubwa tunalosahau ni lishe bora na / mlo kamili. Ukifanya mazoezi ukaendelea kula vyakula vyenye mafuta kwa wingi, hutakuwa umepunguza tatizo. Fanya mazoezi kisha pata maziwa mtindi ujionee tofauti.